Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 137 SAA HERI YA SALA nyimbo za wokovu
1
Saa heri ya sala
Tunapojidhili,
Kama tukija kwake
Yesu rafiki,
Tukiwa na imani
Kwamba yu mlinzi,
Waliochoka sana
Watapata raha.
Saa ya sala,
Iliyo heri.
Waliochoka sana
Watapata raha.
2
Saa heri ya sala,
Ajapo Mwokozi,
Ili awasikie
Watoto wake.
Hutwambia tuweke
Miguuni pake
Mizigo yetu yote;
Tutapata raha.
3
Saa heri ya sala,
Wawezapo kuja
Kwa Bwana Yesu
Wanaojaribiwa
Moyo wake mpole,
Atawarehemu;
Waliochoka sana
Watapata raha.
4
Saa heri ya sala
Tutakapopewa
Mibaraka ya roho,
Tukimwamini;
Kwa kuamini kweli
Hatutaogopa;
Waliochoka sana
Watapata raha.