Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 125 UNIANGALIE nyimbo za wokovu
1
‘Uniangalie’ atwambia.
Yesu aliyetufia,
Msalabani ni uzima,
Hapa utaipata hazina.
Kutazama Kalwari,
Kutazama Kalwari
Nikupewa kuishi
Kuutazama mti.
2
Ninapojaribiwa ghafula,
Shetani atanitega,
Nikitazama msalaba
Nguvu nitaipata kwa Bwana.
3
Msalabani tautazama,
Kila wakati daima,
Ahadi nitategemea
Hivi kabisa sitaanguka.