Nyimbo za wokovu
Wimbo 97 Umesoma Hadithi ya Yesu? Maneno ya wimbo
Umesoma hadithi ya Yesu?
Alisulubiwa;
Deni yako hapo ililipwa
Na damu, kuokoa.
Yesu alikuvunjikia,
Akafa kukufidia;
Pendo lake ndilo la ajabu,
Alikuvunjikia.
Taji ya miiba iliwekwa
Kichwani mwa Bwana;
Kwa adui aliwaombea
Wawe na masamaha.
Umesoma habari ya mwivi
Aliyeangikwa?
Na jinsi alivyomwomba
Na kufarijiwa?
Wajua kwamba kifoni
Kapaza sauti?
Akasema kwamba imekwisha
Utapata kuokoka.