Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 93 Ndiyo Damu Ya Baraka Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 93 Ndiyo Damu Ya Baraka Maneno ya wimbo

 

Ndiyo damu ya baraka ituoshayo wakosa
Kwake Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa,
Nimestahili hukumu, siwezi kujitakasa;
Nioshe katika damu, takuwa safi kabisa.

Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe katika damu;
Takuwa safi kabisa.

Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa Mtini,
Na maumivu si haba yaliyompata chini.
Nataka kijito hicho niende kuoga sasa;
Ndicho kinitakasacho, nami ni safi kabisa.

Safi kabisa; Safi kabisa!
Ndicho kinitakasacho,
Nami ni safi kabisa.

Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu;
Dhambi ni nyingi kabisa, nipate wapi wokovu?
Yesu kijitoni pako naja naamini sasa
Nioshe kwa damu yako, takuwa safi kabisa.

Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe kwa damu yako,
Takuwa safi kabisa.

Exit mobile version