Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 9 Yesu Mfalme Mwokozi Wangu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 9 Yesu Mfalme Mwokozi Wangu Maneno ya wimbo

 

Yesu Mfalme, Mwokozi wangu,
Maisha yangu nimekupa;
Nafurahi kwa wokovu wangu
Damu yako hunifungua.

Mwokozi wangu, Mwokozi wangu,
Ndiwe wa thamani na pendo;
Mwokozi wangu, Mwokozi wangu,
Nimejaa na sifa zako.

kufunguliwa!
Habari Njema!
Madoa yote yamefutwa;
Yesu akaja akae kwangu,
Kwa pendo lake nimewaka.

Yesu Bwana, nimekusujudu,
Hazina zangu ziwe zako;
Unifundishe nikutukuze,
Hata milele niwe wako.

Nifikapo mle mbinguni,
Nitaona uzuri wako;
Nitafurahi hata milele,
Nitakua mfano wako.

Exit mobile version