Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 89 Ewe Kristo, Mwenye Utakaso Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 89 Ewe Kristo, Mwenye Utakaso Maneno ya wimbo

 

Ewe Kristo, Mwenye utakaso,
Utume moto, na utume;
Tumekidai kipawa chako,
Utume moto , na utume:
Utazame waaminifu,
Utupe Roho Mtakatifu;
Kwa Pentekoste twakusifu,
Utume moto, na utume.

Mungu wa Eliya tusikie,
Utume moto, na utume;
Maisha utusaidie,
Utume moto, na utume:
Dhambi zote na uzichome,
Utukufu wako tuuone;
Twataka ili tupinduke,
Utume moto, na utume.

Moto wako tumeulilia,
Utume moto, na utume;
Haja zetu zote zitimie,
Utume moto, na utume:
Kwa nguvu, mema ya kutenda,
Kwa neema twaweza kushinda;
Na uwezo wa kutembea,
Utume moto, na utume.

Exit mobile version