Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 87 Imani Ya Ajabu Yaufurahisha Moyo Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 87 Imani Ya Ajabu Yaufurahisha Moyo Maneno ya wimbo

 

Imani ya ajabu yaufurahisha moyo
Roho akikaa ndani;
Tena, wokovu utatuletea utakaso
Roho akikaa ndani.

Ni Roho Mtakatifu,
Ni Roho Mtakatifu,
Akaapo moyoni, Twakaa wokovuni.
Ni Roho Mtakatifu.

Hakuna tamaa ya anasa ulimwenguni
Roho akikaa ndani,
Uovu na dhambi zote zikachomwa motoni
Roho akikaa ndani.

Hatutaanguka tena bali tutasimama
Roho akikaa ndani,
Hakuna hasira wala kujipendeza tena
Roho akikaa ndani.

Exit mobile version