Nyimbo za wokovu
Wimbo 82 Mungu Alituma Kwangu Maneno ya wimbo
Mungu alituma kwangu nguvu zake,
Niwekwe kila saa na neema yake:
Tangu nilipokaa pamoja na Roho,
Moto wa upendo unachoma moyo.
Moto unawaka, moto unawaka,
Moto wa Mungu , moyoni unawaka;
Roho amekuja, nafurahi sasa,
Moto wa Mungu, moyoni unawaka.
Mbele ya Msalaba najitoa sasa,
Na niwe sadaka kwa Bwana daima;
Gharama ya dhambi, Yesu alilipa,
Na juu ya sadaka moto unawaka.
Ahadi ya Bwana, sasa naishika,
Kwa neema yake nikakubalika;
Utukufu wote ni kwa Bwana Mungu,
Moto wa upendo unawaka kwangu.