Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 77 Namwandama Bwana Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 77 Namwandama Bwana Maneno ya wimbo

 

Namwandama Bwana kwa alilonena,
Njia yangu huning`azia;
Nikimridhisha atanidumisha
Taamini nitii pia.

Amini utii, Njia pekee ni hii
Ya furaha kwa Yesu: Amini ukatii.

Giza sina kwangu wala hata wingu
Yeye mara huviondoa;
Oga, wasiwasi, sononeko, basi;
Huamini nitii pia.

Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipa;
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki.
Taamini nitii pia.

Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote Yesu kumpa;
Napata fadhili na radhi kamili,
Taamini nitii, pia.

Nitamfurahi na kumtumai,
Majumbani na njia – njia;
Agizo hatenda; nikitumwa hwenda,
Huamini, nitii pia.

Exit mobile version