Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 70 Nafurahi Moyoni Mwangu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 70 Nafurahi Moyoni Mwangu Maneno ya wimbo

 

Nafurahi moyoni mwangu,
Yesu ameniambia,
Tulia, usiwe na hofu

Mwendoni mwa maisha.

Yesu, Yesu, Yesu,
Ni jina tamu;
Limeniridhisha ,
Katika mwenendo wangu.

Kwa uovu nilianguka,
katika maisha yangu;
Bali Yesu akanivuta,
Yeye Mwokozi wangu.

Naishi kwa upendo wake,
Kweli, amenipumzisha
Nikimtazama uso wake,
Atanisalimisha.

Nikihangaika njiani,
Yesu ataniongoza
Amenitolea ahadi,
Uchungu atapoza.

Atarudi kutoka mbinguni
Ili anikaribishe,
Na tutapita kwa mawingu,
Ataniwasiilsha.

Exit mobile version