Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 65 Nadumu Kwa Ahadi Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 65 Nadumu Kwa Ahadi Maneno ya wimbo

 

Nadumu kwa ahadi zake Mfalme,
Yesu asifiwe kwa siku zote;
Nitamwimbia sana, atukuzwe,
Kudumu kwa ahadi zake.

Dumu, Dumu,
Nadumu kwa ahadi za Bwana wangu;
Dumu, Dumu,
Nadumu kwa ahadi za Mungu.

Nadumu kwa ahadi, sina shaka,
Ahadi zisizokosa kabisa;
Kwa Neno lake Mungu, nitashinda;
Kudumu kwa ahadi zake.

Nadumu kwa ahadi, nafahamu
Nina utakaso mkamilifu;
Kudumu kwa uhuru wake yesu,
Kudumu kwa ahadi zake.

Nadumukwa ahadi zake Kristo,
Kwa milele nimefungwa na pendo;
Nitashinda kwa upanga wa Roho,
Kudumu kwa ahadi zake.

Nadumu kwa ahadi, sitakosa,
Sauti ya Roho nitasikia;
Katika Mwokozi nimepumzika,
Kudumu kwa ahadi zake.

Exit mobile version