Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 61 Twendeni Askari Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 61 Twendeni Askari Maneno ya wimbo

 

Twendeni askari, watu wa Mungu;
Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.

Ametangulia Bwana vitani,
Twende mbele kwani ndiye amini.

Twendeni askari watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu.

Jeshi la Shetani, likisikia
Jina la Mwokozi, litakimbia,
Kelele za shangwe zivume nchi;
Ndugu, inueni zenu sauti.

Kweli kundi dogo, watu wa Mungu,
La mababa yetu ni letu fungu,
Hatutengwi nao, moja imani,
Tumaini moja, na moja dini.

Haya mbele watu nasi njiani,
Inueni mioyo, nanyi sifuni;
Heshime na sifa ni ya Mfalme,
Juu hata chini, sana zivume.

Exit mobile version