Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 59 Nizidi Yesu Kumjua Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 59 Nizidi Yesu Kumjua Maneno ya wimbo

 

Nizidi Yesu kumjua,
Mapenzi yake kufanya;
Na nizidi kuzijua
Pendo na wokovu pia

Zaidi ya Yesu
Zaidi ya Yesu,
Nizidi kumjua sana
Pendo na wokovu pia.

Nizidi nielimishwe,
Mapenzi yake nitende;
Roho wa Mungu, na uwe,
Mwalimu wangu milele.

Nizidi katika neno,
Kushirikiana nalo;
Niisikie sauti,
Misemo iwe moyoni.

Nizidi kumwona Yesu,
Na utukufu wake mkuu;
Uzidi ufalme wake
Hata kurejea kwake.

Exit mobile version