Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 55 Sioni Haya Kwa Bwana Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 55 Sioni Haya Kwa Bwana Maneno ya wimbo

 

Sioni haya kwa Bwana
Kwake nitang`ara!
Mti wake sitakana
Ni neno imara!

Msalaba ndio asili ya mema,
Nikatua mzigo hapo:
Nina uzima, furaha daima Njoni kafurahini papo.

Kama kiti chake vivyo
Ni yake ahadi:
Alivyowekewa navyo
Kamwe havikomi.

Bwana wangu, tena Mungu
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu
Wala kunikana.

Atakiri langu jina
Mbele za Babaye:
Anipe pahali tena
Mbinguni nikae.

Exit mobile version