Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 54 Nilitembea Gizani Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 54 Nilitembea Gizani Maneno ya wimbo

 

Nilitembea gizani,
Yesu akaona;
Kwa mwanga wa pendo lake,
Giza lilifutwa.

Mwanga, mwanga rohoni mwangu,
Mwanga, mwanga kwa njia yangu;
Tangu nimepata wokovu wangu,
Yesu amenijaza kwa mwanga mkuu.

Ninapoenda nuruni,
Mwa upendo wake;
Nashirikiana naye,
Gizani si kwake.

Nikitembea shambani
Ama kwa njiani;
Naona mavuno yake,
Anifanye mvuni.

Atakaporudi tena,
Sitaki kutanga;
Nitamwona Yesu Bwana,
Yeye ndiye Mwanga.

Exit mobile version