Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 47 Akifa Yesu Nikafa Naye Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 47 Akifa Yesu Nikafa Naye Maneno ya wimbo

 

Akifa Yesu nikafa naye,
Uzima upya uishi naye;
Humtazama mpaka aje:
Nyakati zote ni wake Yeye.

Nyakati zote nimo pendoni,
Nyakati zote ni Uzimani,
Humtazama hata atokee,
Nyakati zote mimi ni wake.

Vita sipigi visivyohaki,
Na Bwana Mungu hapiganiki;
Beramu yake haitwaliki,
Napo popote hila sitaki.

Sina mashaka, akawa mbali;
Mizigo yote aihimili;
Ananituliza Emanweli,
Nyakati zote mimi husali.

Sina huzuni na mimi sidhii:
Simwagi chozi, wala siguni:
Sikuti afa, ila kitini
Daima hunifikiri mimi.

Kila unyonge huusikia:
Kila ugonjwa kwake hupoa;
Yesu ni Mwenye kuniokoa
Nyakati zote hunijalia.

Exit mobile version