Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 46 Mpendao Bwana Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 46 Mpendao Bwana Maneno ya wimbo

 

Mpendao Bwana
Ije raha yenu!
Imbeni nyimbo za raha (2)
Wa ibada yenu. (2)

Twenenda Zayuni,
Mji mzuri Zayuni;
Twenenda juu Zayuni,
Ni masikani ya Mungu.

Wasiimbe wao
Wasioamini,
Watoto wa Mungu ndio (2)
Waimbao chini. (2)

Twaona rohoni
Baraka za Mungu,
Tusijafika mbinguni (2)
Kwenye utukufu. (2)

Tutakapomwona
Masumbuko basi,
Tusijafika mbinguni (2)
Anasa halisi. (2)

Tupaze sauti,
Na yeshe machozi;
Twenenda kwa Imanweli (2)
Naye ni Mwokozi. (2)

Exit mobile version