Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 45 Uje Unisaidie Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 45 Uje Unisaidie Maneno ya wimbo

 

Uje unisaidie,
Mwokozi wa Baraka;
Rehema yako ni tele,
Nikutolea sifa:
Unifundishe kusifu,
Sifa za malaika;
Nimekaa upendoni,
Upendo wa hakika.

Naja kwako unishike,
Najitoa kabisa;
Kwa mapenzi yako niwe,
Mwaminifu wa sifa:
Nilipotembea mbali,
Yesu alinipata;
Akaniokoa kweli,
Kwa damu ya salama.

Kwako nimekuwa mdeni,
Umenipa neema;
Nisipotelee mbali,
Unifunge kwa wema:
Ni mwenye kutangatanga,
Ni mwenye kupotea;
Unichukue moyo wangu,
unifunge kabisa.

Exit mobile version