Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 44 Rehema ya Baba Yetu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 44 Rehema ya Baba Yetu Maneno ya wimbo

 

Rehema ya Baba yetu,
Yang`aza nchi yake;
Lakini ametuweka
Tuwe walizi wake.

Taa zenu na ziwake,
Nuru zenu tumeni;
Msafiri asizame,
Mwokoeni majini.

Giza ya dhambi twaona,
Mawimbi twasikia;
Wengine wanatafuta
Nuru za kutulia.

Taa zitengenezeni,
Mwokoeni msafiri;
Aangukaye majini,
Na asife gizani.

Exit mobile version