Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 43 Rafiki Wa Yesu Ndimi Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 43 Rafiki Wa Yesu Ndimi Maneno ya wimbo

 

Rafiki wa Yesu ndimi,
Niliye dhaifu;
Ninaye Rafiki mwema,
Aliyekomboa.

Yesu Mshirika,
Rafiki yangu;
Ushirika mtakatifu,
Ndiye Rafiki yangu.

Urafiki wa daima,
Usiopunguka;
Yesu anipa amani,
Yu Mwenye hakika.

Aniongoza gizani,
Aijua njia;
Anilinda maishani,
Aliyenifia.

Nikishikwa na ugonjwa.
Ataniinua;
Kifo nikikaribia Ataniongoza.

Yesu ni Rafiki Mwema,
Humu duniani;
Yeye atanichukua Mpaka mbinguni.

Exit mobile version