Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 42 Niwonapo Mti Bora Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 42 Niwonapo Mti Bora Maneno ya wimbo

 

Niwonapo Mti bora
Kristo aliponifia
Kwanfu pato ni hasara,
Kiburi nakichukia.

Na nisijivune, Bwana,
Ila kwa mauti yako;
Upuzi sitaki tena,
Zi chini ya damu yako.

Tangu kichwa hata nyayo
Zamwangwa pendo na hamu,
Ndako pweke hamu hiyo,
Pendo zako zimetimu.

Vitu vyote vya dunia
Si sadaka ya kutosha;
Pendo zako zaniwia
Nafsi, mali, na maisha.

Exit mobile version