Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 36 Mwokozi Alinifia Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 36 Mwokozi Alinifia Maneno ya wimbo

 

Mwokozi alinifia,
Yesu Mfalme wangu;
Akajitoa kabisa,
Kwa niaba yangu.

Mwokozi, nisaidie
Niwe mwaminifu;
Utakapomiliki juu,
Bwana, nikumbuke.

Aliugue mtini,
Kwa maovu yote;
Alikufa hapa chini,
Tuokoke sote.

Nijifiche uso wangu,
Nione msalaba;
Nimpe shukrani yangu,
Astahili sifa.

Sina uwezo kulipa,
Deni ya upendo;
Bali Yesu, najitoa,
Nitumike kwako.

Exit mobile version