Nyimbo za wokovu
Wimbo 35 Yesu Kwetu Ni Rafiki Maneno ya wimbo
Yesu kwetu ni rafiki,
Hwambiwa haja pia;
Tukiomba kwa Babaye
Maombi asikia;
Lakini twajikosesha,
Twajitweka vibaya;
Kwamba tukimwomba Mungu,
Dua atasikia.
Una dhiki na maonjo?
Una mashaka pia?
Haifai kufa moyo,
Dua atasikia.
Hakuna mwingine Mwema
Wakutuhurumia:
Atujua tu dhaifu;
Maombi asikia.
Je, hunayo hata nguvu,
Huwezi kwendelea,
Ujapodharauliwa
Ujaporushwa pia.
Watu wangekudharau,
Wapendao dunia,
Hukwambata mikononi,
Dua atasikia.