Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 33 Wakati Wangu Kuomba Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 33 Wakati Wangu Kuomba Maneno ya wimbo

 

Wakati wangu kuomba,
Umenialika kusala;
Nimsihi Mungu Mwenyezi,
Anitulize kwa mapenzi,
Nyakati za shaka nyingi
Nipate ufadhili,
Kwa wewe nitangojea,
Ewe, wakati wa kuomba.

Wakati wangu kuomba,
Umeniletea furaha,
Pamoja nao wenzangu,
Nashirikiana na Mungu.
Mahali hapa nikae,
Uso wa Mungu, nimwone;
Kwako nitakungojea,
Ewe, wakati wa kuomba.

Wakati wangu kuomba,
Mabawa yako hunishika;
Kwa Yesu aliye kweli,
Aningojea kubariki.

Tangu alinialika
Nimwamini kwa hakika,
Kwa wewe nitangojea,
Ewe, wakati wa kuomba.

Exit mobile version