Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 31 Peleleza Ndani Yangu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 31 Peleleza Ndani Yangu Maneno ya wimbo

 

Peleleza ndani yangu,
Iwe safi nia,
Kwangu kama kwako Mungu
Idhihiri pia.

Peleleza Moyo wangu
Unifunulie,
Yaliyomo ndani yangu
Nami niyajue.

Kwanza washe zako tambi,
Kumefunga giza;
Nijue ambavyo dhambi
Ni la kuchukiza.

Peleleza na mawazo,
Ni mbegu za mambo,
Asili ya machukizo,
Maumbuo – umbo.

Zidi kuyapeleleza
Katikati yangu
Hata wishe nifundishe nifundishe
Udhaifu wangu.

Hapo nikikwinamia
Mbele zako, Mungu,
Hakika nitakujua
U mpenzi wangu.

Exit mobile version