Nyimbo za wokovu
Wimbo 3 Uniumegee Mkate Hai Maneno ya wimbo
Uniumegee Mkate Hai,
kama ulivyomega zamani,
Ninakutafuta, Ewe Bwana,
Roho yangu yakutaka sana.
Uniumegee Mkate Hai,
Neno lako likae moyoni,
Mawzo ya ndani, yawe safi,
Niongozwe daima, Mwokozi.
Neno lako Bwana, nilione,
Ujumbe wako niandikie;
Tushirikiane na upendo,
Uniitilie sura yako.