Nyimbo za wokovu
Wimbo 29 Kwa Mfano Wako Maneno ya wimbo
Kwa mfano wako, Mwokozi wangu,
Hiyo ni tumaini langu;
Mali za dunia nitatoa,
Nipate mfano kama Yesu.
Kwa mfano wako, Kwa mfano wako,
Ewe Mkombozi , niwe wako;
Unitilie muhuri yako,
Nigeuke kwa mfano wako.
Kwa mfano wako, Mwenye huruma,
Kusamehe na kuwa mwema;
Waangukao niwainue,
Wenye dhambi niwatafute.
Kwa mfano wako, Roho mpole,
Mtakatifu, Mvumilivu;
Kila kemeo kustahimili,
Mateso yote nikubali.
Kwa mfano wako, ninakujia,
Nipakwe na mafuta yako;
Nakuletea uzima wangu,
Tangu sasa na niwe wako.
Kwa mfano wako, nakusihi,
Unimwagie Roho yako;
Niwe hekalu, ukae ndani,
Nistahilishe pendo lako.