Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 28 Mungu Msaada Wetu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 28 Mungu Msaada Wetu Maneno ya wimbo

 

Mungu msaada wetu
Tangu miaka yote,
Ndiwe Tumaini yetu
Ya zamani zote.

Kivuli cha kiti chako
Ndiyo Ngome yetu,
Watosha mkono wako
Ni ulinzi wetu.

Kwanza havijakuwako
Nchi na milima,
Ndiwe Mungu; chini yako
Twakaa salama.

Na miaka elfu ni kama
Siku moja kwako;
Utatulinda daima
Tu wenyeji wako.

Ila Wewe Mungu wetu,
Ndiwe wa kudumu;
Ndiwe bora, Ngome yetu
Twakaa dawamu.

Exit mobile version