Nyimbo za wokovu
Wimbo 24 Yesu Unipendaye Maneno ya wimbo
Yesu unipendaye,
Kwako nakimbilia,
Niwewe utoshaye
Mwovu akinijia;
Yafiche ubavuni
Mwako maisha yangu;
Nifishe bandarini;
Wokoe moyo wangu.
Ngome nyingine sina;
Nategemea kwako.
Usinitupe Bwana,
Nipe neema yako,
Nsha kukwamania,
Mwenyekuniwezesha;
shari wanikingia,
Vitani wanitosha.
Nakutaka mpaji,
Vyote napata kwako;
Niwapo muhitaji,
Utanijaza vyako;
Nao waangukao Wanyonge wape nguvu;
poza wauguao,
Uongoze vipofu.
Bwana umenisha
Moyo kwa damu yako;
Neema ya kutosha
Yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona
Kisima cha uzima;
Mwangu moyoni Bwana,
Bubujika daima.