Nyimbo za wokovu
Wimbo 23 Yesu Unihifadhi Maneno ya wimbo
Yesu unihifadhi
Hapa Msalabani;
wajiao Kalvari,
Waponywe Damuni
Msalaba, Msalaba,
Humu nina sifa;
Hata nitapumzika,
Mahali pa raha.
Karibu na Msalaba
Nimepatikana,
Na pendo na neema
Nimezungukiwa.
Karibu na Msalaba
Na Mwana wa Mungu;
Nitatembea naye,
Aliye mtukufu.
Karibu na Msalaba Nitakesha sana;
Hata nitawasili
Mbinguni kukaa.