Nyimbo za wokovu
Wimbo 210 Upendo Wa Yesu Ni Wa Ajabu Maneno ya wimbo
Upendo wa Yesu ni wa ajabu,
Alitoka mbinguni;
Akashuka kuonja umaskini,
Akateswa hapo msalabani.
Upendo, nilioupewa,
Neema, isiyopunguka;
Upendo, Upendo,
Nitautangaza upendo.
Si kwa haki yangu niliyotenda.
Bali kwa pendo lake;
Sistahili neema wala pendo
Yesu hunipa wokovu wake.
Yesu atanilinda safarini,
Kwa maishani mote;
Sitaona shaka wala hasara,
Anatimiza ahadi zote.