Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 21 Ni Wako Wewe, Nimekujua Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 21 Ni Wako Wewe, Nimekujua Maneno ya wimbo

 

Ni wako wewe, nimekujua,
Na umeniambia;
Lakini Bwana, nataka kwako
Nizidi kusongea.

Bwana vuta, vuta, nije nisongee,
Sana, kwako mtini.
Bwana vutaa, vuta, nije nisongee,
Pa damu ya thamani.

Niweke sasa nikatumike,
Kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende
Nizidi kukwandama.

Nina furaha tele kila saa,
Nizungumzapo kwako,
Nikuombapo, nami napata,
Kujua nia yako.

Mapenzi yako hayapimiki,
Ila ng`ambo ya liko.
Anasa pia sitazijua,
Bila kufika kwako.

Exit mobile version