Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 209 Nafikiri Juu Ya Kalvari Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 209 Nafikiri Juu Ya Kalvari Maneno ya wimbo

 

Nafikiri juu ya Kalvari,
Naona watu wengi
Waliomdharau Bwana wangu
Alipokufa mtini.

Aleluya, Aleluya,
Kumbuko lenye heri;
Nafikiri juu ya Kalvari;
Nafikiri – fikiri juu ya Mwokozi

Nafikiri juu ya Kalvari,
Naona Msalaba;
Na Bwana wangu akiangikwa
Katikati ya wevi.

Nafikiri juu ya Kalvari,
Tumai la milele;
Dhambi ziliondolewa hapo,
Sasa ninafurahi.

Exit mobile version