Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 206 Una Nafasi Kwa Yesu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 206 Una Nafasi Kwa Yesu Maneno ya wimbo

 

Una nafasi kwa Yesu?
Aliyeondoa dhambi;
Abishapo mlango wako,
Umkaribishe ndani.

Nafasi kwa Mfalme Yesu,
Neno lake ulitii;
Ufungue moyo wako,
Aingie moyoni.

Anasa ina nafasi,
Bali Yesu hawezi;
Kuingia moyo wako,
Mbona wewe humpendi?

Una nafasi kwa Yesu?
Leo akikuita
Usimkatae, mwenzangu,
Ni bora kumwitika.

Exit mobile version