Nyimbo za wokovu
Wimbo 200 Najua Jina Niliheshimulo Maneno ya wimbo
Najua jina niliheshimulo,
Lanipendeza rohoni mwangu;
Jina thamani kupita hesabu,
Yesu ndilo jina la ajabu.
Moyo wangu umependezwa sana,
Nikukumbukapo jina la Kristo;
Sina jina jingine liwezalo,
Kunipatia wokovu nalo.
Jina hili huniletea raha,
Huondoa sikitiko langu;
Huimarisha aliyelemewa,
Jina hilo huponya kabisa.
Jina hilo litadumu milele.
Nguvu zake hazibadiliki;
Jina hilo linang`ara daima,
Jina la Yesu halipunguki.