Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 2 Jina La Yesu, Salamu! Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 2 Jina La Yesu, Salamu! Maneno ya wimbo

 

Jina la yesu, salamu!
Lisujudieni,
Ninyi mbinguni hukumu
Na enzi mpeni.

Enzi na apewe kwenu,
watetea dini
Mkuzeni Bwana wenu
Na enzi mpeni

Enyi mbegu ya rehema
Nanyi msifuni;
Mmeponywa kwa neema,
Na enzi mpeni

Wenye dhambi kumbukeni
Ya Msalabani
Kwa furaha msifuni
Na enzi mpeni

Sisi na wao pamoja
Tu mumo sifani
Milele sifa ni moja,
Ni Enzi mpeni.

Exit mobile version