Nyimbo za wokovu
Wimbo 199 Mungu Wangu,Ndiye Na Mwamini Maneno ya wimbo
Mungu wangu, ndiye namwamini,
Po pote nilipo duniani;
Lo lote lanijialo,
Baba yangu hunitunza humo.
Namwamini Mungu hunipenda Katika dhiki ama mashaka;
Matesoni hunilinda,
Baba yangu hunitunza sana.
Mungu hulinda viumbe vyake,
Huviongoza njiani mwake;
Najua anikumbuka,
Baba yangu hunitunza sana.
Njia ijapokuwa gizani,
Kodnoo hawasahauliwi;
Mungu Mchunga aongoza Baba yangu hunitunza sana.