Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 198 Mungu Baba Yangu, U Mwaminifu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 198 Mungu Baba Yangu, U Mwaminifu Maneno ya wimbo

 

Mungu Baba yangu, U Mwaminifu,
Hakuna geuzo ndani yako;
Hubadiliki, wewe ndiwe sawa,
Jana, leo na siku zijazo.

Wewe Mwaminifu, Wewe Mwaminifu,
Kila siku fadhili napewa;
Vitu vyote ninavyo umenipa
Wewe Mwaminifu kwangu Bwana.

Na viumbe vyote hulingamana,
Kuonyesha utukufu wako;
Jua, na mvua, mwezi tena nyota Hulishuhudia pendo lako.

Samaha la dhambi, tena amani,
Hivi vyote ni baraka zako;
Nguvu zako zitadumu milele,
Nimebarikiwa sasa kwako.

Exit mobile version