Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 194 Yesu Bwana Wangu Ananipenda Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 194 Yesu Bwana Wangu Ananipenda Maneno ya wimbo

 

Yesu Bwana wangu anipenda,
Nguvu zote hazitatutenga;
Akatoa uzima wake,
Niwe mali yake.

Yesu ni Bwana wangu,
Mimi mali yake;
Si kwa muda wa miaka tu,
Bali kwa milele.

Nilipotea mbali dhambini,
Yesu akaja toka mbinguni;
Akanivuta na pendo lake,
Niwe mali yake.

Furaha tele, nimeokoka,
Kutoka dhambi nimefunguka:
Akaniponya kwa damu yake,
Niwe mali yake.

Exit mobile version