Nyimbo za wokovu
Wimbo 192 Mwokozi Niongozwe Maneno ya wimbo
Mwokozi niongozwe
Nisipotee kamwe;
Nina salama kwako,
Nikae nawe pako.
Yesu, Yesu,
Niongoze nisipotee;
Maisha yangu yote,
Mwokozi unishike.
Ee, kimbilio langu,
Wakati dhoruba kuu;
Nina salama yako
Kutegemea kwako.
Mwokozi unishike,
Hata nichukuliwe;
Mpaka nchi ya mwanga,
Mle chozi hapana.