Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 187 Yuko Mwokozi Wa Ajabu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 187 Yuko Mwokozi Wa Ajabu Maneno ya wimbo

 

Yuko Mwokozi wa ajabu,
Alinifia mtini;
Na alitumwagia damu,
Tuokoke, wenye dhambi.

Alinisulubishiwa,
Alinisulubishiwa;
Akafa mtini pa Kalvari,
Alinisulubishiwa.

Alitoka kwake mbinguni,
Mapenzi ayatimize;
Akazaliwa na bikira,
Mfano wa mtu avikwe.

Akapigwa kwa Dhambi zetu,
Akachukua taabu;
Yu Mpozi wa ugonjwa wetu,
Hayo alifanya kwetu.

Kwa wengine akajitoa,
Alipoondoa dhambi;
Makao atutayarisha,
Tuingie mbinguni.

Exit mobile version