Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 184 Nichunguze Mungu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 184 Nichunguze Mungu Maneno ya wimbo

 

Nichunguze, Mungu unijue,
Unijaribu niangalie;
Zitambue dhambi zangu zote,
Unitakase na uniweke.

Nakusifu, umenisafisha,
Neno lako litimike sasa;
Unijaze na moto wa mbingu,
Unipe matumaini yangu.

Unitwae, kweli niwe wako,
Unijaze na upendo wako;
Uondoe kiburi na choyo,
Bwana, nakujitolea moyo.

Mungu Roho, una ufufuo,
Kwangu ianzishe kazi yako;
Haja zote zitapatikana.

Bwana, naomba kwako baraka.

Exit mobile version