Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 182 Kijito Cha Utakaso Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 182 Kijito Cha Utakaso Maneno ya wimbo

 

Kijito cha utakaso
Ni damu ya Yesu,
Bwana anao uwezo
Kunipa wokovu.

Kijito cha utakaso,
Nizame kuoshwa humo;
Namsifu Bwana kwa hiyo,
Nimepata utakaso.

Viumbe vipya naona,
Damu ina nguvu;
Imeharibu uovu,
Uliodhulumu.

Naondoka kutembea Nuruni mwa mbingu,
Na moyo safi kabisa
Kumpendeza Mungu.

Ni neema ya ajabu,
Kupakwa na damu;
Na Bwana Yesu kumjua,
Yesu wa Msalaba.

Exit mobile version