Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 180 Karibu Nawe, Ee Mwokozi Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 180 Karibu Nawe, Ee Mwokozi Maneno ya wimbo

 

Karibu nawe, Ee Mwokozi,
Univute Bwana wa thamani;
Unikaribishe Moyoni,
Uniweke kwako salamani,
Uniweke kwako salamani.

Karibu nawe, sina kitu,
Sikuiletea sadaka kuu;
Nakujitolea kabisa,
Kwa damu nipate kutakaswa,
Kwa damu nipate kutakaswa.

Karibu nawe, Bwana wangu,
Niliuacha uovu wangu;
Kiburi changu na anasa,
Namtaka Yesu aliye Bwana,
Namtaka Yesu aliye Bwana.

Karibu nawe, hata mwisho,
Nina salama ndani ya Kristo;
Mwokozi wangu kwa milele,
Nitakuwa karibu na wewe,
Nitakuwa karibu na wewe.

Exit mobile version