Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 178 Baba Yangu Ana Mali Nyingi Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 178 Baba Yangu Ana Mali Nyingi Maneno ya wimbo

 

Baba yang ana mali nyingi,
Hushika hazina zote mkononi;
Fedha zote na mawe thamani,
Na dhahabu zote ulimwenguni.

Ni mwana wa Mfalme,
Mwana wa Mfalme;
Pamoja na Yesu,
Ni mwana wa Mfalme.

Mwana wa Baba, Mwokozi wangu,
Alitembea humu ulimwengu;
Bali anatuombea saa,
Ili tuwe watu wake kabisa.

Nilitupwa mbali duniani,
Nikakubali kuwa mwenye dhambi;
Bali sasa nimeokolewa,
Kweli, jina langu limeandikwa.

Hema au nyumba, sioni shaka,
Makao mazuri nitayapata;
Nikihamishwa na watu wangu,
Nitafurahi na Mwokozi wangu.

Exit mobile version