Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 173 Nimehitaji Mwokozi Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 173 Nimehitaji Mwokozi Maneno ya wimbo

 

Nimemuhitaji Mwokozi,
Awe nami daima;
Nataka mikono yake
Kunizunguka sana.

Hofu rohoni sina,
Aniongoze tena;
Sitanung`unika tena,
Nimfutate daima.

Nimehitaji Mwokozi,
Sina imani nyingi;
Atanifufusha moyo,
Wengine hawawezi.

Nimehitaji Mwokozi,
Mwenendoni mwa maisha;
Katika matesa mengi,
Tena katika vita.

Nimehitaji Mwokozi,
Kiongozi njiani;
Kwa jicho aniongoze Nifike mbinguni.

Exit mobile version