Nyimbo za wokovu
Wimbo 168 Mungu Alipenda Ulimwengu Maneno ya wimbo
Mungu alipenda ulimwengu,
Akamtoa Mwana wake;
Kila mtu amwaminiye,
Na uzima apate.
Ni kweli ndiyo kweli,
Ahadi zake zi kweli;
Neno lake Mungu ladumu,
Ahadi zake zi kweli.
Nikawa mwana asiye mwema,
Kwa dhambi nikawa mtumwa;
Hata nikapata baraka
Iliyonipendeza.
Neno la Bwana nikakubali
Aliposema na mimi;
Ahadi nikazisadiki,
Nikatengwa na dhambi.
Ninao uzima wake Mungu,
Moyo wangu umejazwa;
Na nitamsifu Bwana Yesu
Aliyenikomboa.