Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 161 Jua Kila Lingarapo Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 161 Jua Kila Lingarapo Maneno ya wimbo

 

Jula kila ling`arapo
Yesu atashinda huko
Mfalme wa nchi zote,
Hata dunia iishe.

Na daima aombewe,
Atawazwe na majumbe,
Kama udi jina lake
Na sadaka tupeleke.

Kila lugha na taifa
Watamwimbia na sifa,
Na Jina lake vijana
Vitalitukuza sana.

Ashindapo ni furaha
Kwa waovu msamaha;
Huacha huru wafungwa,
Wahitaji hushibishwa.

Watu wote na wasifu,
Wampe na utukufu;
Malaika, watu nao
Wamwimbie sifa zao.

Exit mobile version