Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 159 Kichwa Kilivikwa Miiba Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 159 Kichwa Kilivikwa Miiba Maneno ya wimbo

 

Kichwa kilivikwa miiba,
Kina enzi sasa;
Anayo taji ya sifa,
Ilivyompasa.

Pake ni juu sana
Jumbe wa wajumbe;
Yesu, Bwana wa mabwana,
Nuru za viumbe.

Nyemi za wakaao juu,
Nyemi za wa chini,
Alionya pendo kuu,
Jina la sirini.

Mti wa aibu sana
Kwao una wema;
Wanayo raha daima
Kwa kifo cha Bwana.

Chini wanayo dhiki kuu;
Kwako wana enzi;
Kwao furaha, pato kuu
Ni yake mapenzi.

Mti wa kufa kwa Yesu
Kwetu ni uzima;
Mali, na tumai letu
Tunu ya neema.

Exit mobile version