Nyimbo za wokovu
Wimbo 155 Usiku Mkuu! Maneno ya wimbo
Usiku mkuu! Mtakatifu!
Uko utulivu;
Bikira amezaa Mwana,
Mtoto Mtakatifu ni Bwana;
Alale amanini, Alale amanini.
Usiku mkuu! Mtakatifu!
Wachunga wa hofu;
Waliogopa kuwaona
Malaika walipoimba;
Kristo amezaliwa, Kristo amezaliwa
Usiku mkuu!
Mtakatifu!
Ni Mwana wa Mungu;
Ametuletea neema,
Ili tukae na salama;
Yesu Kristo Mwokozi, Yesu Kristo Mwokozi.